Full-Width Version (true/false)


Uhuru Seleman afunguka kukamatwa na Bastola chini Afrika Kusini
Nyota wa Tanzania Uhuru Seleman anayekipiga kwenye klabu ya Mthatha Bucks, inayocheza ligi daraja la kwanza nchini Afrika Kusini, amefunguka juu ya suala lililowahi kuwa ngumzo la kukamatwa na Bastola na mamlaka za usalama nchini humo. 
Akiongelea suala hilo kwa mara ya kwanza kwenye mahojiano na eatv.tv Uhuru amesema, sio kweli kwamba alikamatwa bali ni silaha anayoimiliki kwa mujibu wa sheria na alichelewa kuilipia ndio mana mamlaka zikamuita.

''Kilichotokea sio kwamba nilikamatwa, ile silaha naimiliki kwa kufuata sheria na taratibu zote ila nilichelewa kuilipia nikaitwa na kwa mujibu wa taratibu ni lazima niiache kwanza kisha nifuatilie malipo nikikamilisha niichukue na nilifanya hivyo'', amesema.

Aidha Uhuru ameongeza kuwa maisha ndani ya Afrika Kusini yanakulazimu uwe na ulinzi wako binafsi kwani watu wa huko wanapenda fujo sana na ndio maisha yao halisi hivyo inashauriwa kujilinda mwenyewe.

Kwa upande mwingine Uhuru amesema soka nchini humo linalipa na watu wanaheshimu wachezaji na vipaji vyao kama waigizaji na wasanii, tofauti na Tanzania ambapo mashabiki wanaweza kukuukana tu bila hata kukujua.

No comments

Powered by Blogger.