Full-Width Version (true/false)


Ujerumani yamtangaza, Manuel Neuer kuwa nahodha wa timu ya taifaMlindalango wa klabu ya FC Bayern Munich, Manuel Neuer amekabidhiwa kitambaa cha unahodha ndani ya timu ya taifa ya Ujerumani.


Neuer amekabidhiwa majukumu hayo hii leo wakati Kocha Mkuu wa timu hiyo, Joachim Low akikitangaza kikosi cha wachezaji 23 watakao iwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi huu nchini Urusi.

Hata hivyo watu wengi walishitushwa na kitendo cha kutolewa kwenye kikosi cha timu hiyo Winga machachari wa klabu ya Manchester City,  Leroy Sane.

Mtandao wa kijamii wa Twitter wa Shirikisho la soka nchini Ujerumani lilianika jina la Leroy Sane na wenzake watatu kuachwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 watakao kwenda Urusi.

Msimu uliyopita, Sane alichukua tuzo ya mchezaji mdogo wa kulipwa wa mwaka ligi kuu ya nchini Uingereza (PFA) akiwa anaitumikia klabu yake ya Manchester City.

No comments

Powered by Blogger.