Full-Width Version (true/false)


Ukweli kuhusu mjengo mpya wa Aslay na kusaini King Empire


Meneja wa msanii Aslay, Chambusso amefunguka kuhusu muimbaji huyo kununua mjengo wa ghorofa na kusaini King Empire.
Chambusso amesema yeyote anayeona mafanikio ya msanii huyo ni kutokana na kazi za muziki hadi sasa, pia alikanusha kuwa mjengo ameupata baada ya kusaini label ya King Empire.

“Ukimuona Aslay ana kimjengo, ana gari nzuri anafanya show ana kazi zake zinazoendelea,” Chambuso ameaimbia EATV. 

Kuhusu iwapo Aslay amesaini King Empire, Chambuso alisema bado ni mapema kuweka wazi hilo ila kuna mambo yanakuja.

“Kuna vitu vinakuja hatuwezi kuongea, King Empire inakuja inamiliki wasanii kama watano hivi. Inawekana kwa msanii yeyote kwa sababu mimi nipo King Empire, kwa hiyo lolote inaweza kutokea, Aslay awepo au asiwepo,” alisema.

Utakumbuka October 31, 2017 aliweka wazi kukabidhiwa gari aina ya BMW na menejimenti yake. Haikuwa gari ya kwanza kwa Aslay kuipata kutoka kwenye muziki, May 2015 alikabidhiwa gari na menejimenti ya Mkubwa Fella aliyokuwa akifanya nayo kazi kwa kipindi hicho.

No comments

Powered by Blogger.