Full-Width Version (true/false)


Umeme Gridi ya Taifa kutoka MakambakoSongea kuokoa Bilioni 20.


Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani amemuagiza Mkandarasi anayejenga kituo cha kupoozea umeme cha madaba mkoani Ruvuma, ambacho kitapokea umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Makambako mkoani Njombe kwenda Songea mkoani Ruvuma, kukamilisha ujenzi wakituo hicho hadi ikapo Septemba mwaka huu ili kuipunguzia gharama kubwa shirika la TANESCO mkoani Ruvuma ambalo linatumia zaidi ya shilingi Bilioni 20 kwa mwaka kwa ajili ya kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme. 

Akiongea mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha kupoozea umeme wa Gridi ya Taifa cha Madaba ambacho kitapokea umeme kutoka Makambako mkoani Njombe kwenda Songea mkoani Ruvuma,Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani amesema kwa sasa Shirika la ugavi wa umeme (TANESCO) mkoa wa Ruvuma linatumia gharama kubwa mno kwa ajili ya kununua mafuta ya kufua umeme hivyo mradi huo ukikamilika mapema utasaidia kuondoa gharama hizo. 

Hata hivyo Meneja wa Shirika la TANESCO mkoa wa Ruvuma,Mhandisi Frolence Mwakasege, amesema kwa halmashauri ya Madaba licha ya kuwa na mashine mpya ya kufua umeme inayotumia mafuta lakini changamoto kubwa ni baadhi ya wananchi wanahohitaji umeme kukosa kusuka waya za umeme kwenye nyumba zao.

No comments

Powered by Blogger.