Full-Width Version (true/false)


Usajili wa Tiba John kutoka Ndanda kwenda Singida united wazua zengwe lenye utataUongozi wa klabu ya Ndanda FC ya Mtwara umewapiga mkwara Singida United kuhusiana na mchezaji Tiber John George waliomtangaza jana kuingia naye mkataba wa miaka mitatu.


Afisa Habari wa Ndanda, Idrisa Bandari, amefunguka kwa kusema kuwa Singida wamemchukua mchezaji huyo kinyemela bila kufuata taratibu zinazotakiwa.


Bandari ameeleza kuwa Tiber alikuwa ana mkataba wa miaka mitatu na Ndanda na walimkuza kutoka kikosi cha pili hivyo si busara kwa Singida United kumchukua bila mazungumzo.


Licha ya hayo, Bandari amesema kuwa anaamini Singida United ni watu wastaarabu na waungwana akieleza ana imani watakuja na kukaa mezaji ili wayamalize.


George alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotambulishwa jana na Singida jijini Arusha mbele ya Waandishi wa Habari, akiwemo Mbrazil Oliveria dos Santos.

No comments

Powered by Blogger.