Full-Width Version (true/false)


Wabunge kupimwa VVU kabla ya kuanza kazi
BAADHI ya wabunge wameishauri serikali kuweka utaratibu ambao utalazimisha watu wa makundi maalum, wakiwamo wabunge wanapochaguliwa kupimwa Virusi vya Ukimwi (VVU) kabla ya kuanza kutumikia wapigakura wao. 

Ushauri huo waliutoa juzi walipokuwa wakichangia mada mbalimbali kwenye semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati za Bunge za Ukimwi na Dawa za Kulevya na Kamati ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Ukimwi bungeni. 

Akichangia katika mjadala huo, Mbunge wa Makete (CCM), Norman Sigalla, alisema ili kukabiliana na maambukizi ya VVU, ni vyema ikawa lazima makundi mbalimbali wakiwemo wabunge na wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu kupima afya zao. Sigalla alisema hatua hiyo itasaidia kujua hali ya maambukizi kwa makundi mbalimbali kwa kupata takwimu sahihi. 

Aidha, alisema Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids) ifanye uchunguzi wa kina wa chanzo halisi cha kiwango kikubwa cha VVU katika Mkoa wa Njombe ikilinganishwa na mikoa mingine yenye mabinti wengi wadogo waliojiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi, ikiwamo Lindi. 

Alisema utafiti uliofanyika mwaka 2016/17, ulionyesha kuwa kiwango cha maambukizi katika mkoa wa Njombe ni asilimia 11.4 huku mwaka 2012/13 kilikuwa asilimia 14.8 wakati Lindi na Zanzibar kiwango chake ni kidogo. 

 “Unakuta mikoa ya wenzetu kule kama Lindi binti mdogo wa darasa la sita au la saba tayari wanajua mapenzi lakini kwa mkoa wa Njombe binti wa umri huo bado ni bikra, lakini wao wenzetu kiwango cha maambukizi eti ni kidogo. Hili suala liangaliwe ili tujue sababu hasa za Njombe kuwa na kiwango kikubwa huku Lindi na Mtwara wakiwa na kiwango kidogo,” alisema. 

Naye Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene, alisema utaratibu huo wa kupima makundi maalum tayari uko kwa wanajeshi na polisi, hivyo si vibaya na makundi mengine kufanya hivyo. 

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba nijazilizie hapo hapo kwa Sigalla kuwa utaratibu huu tayari unafanyika kwa makundi mengine kama ya polisi na wanajeshi, hivyo ni vizuri tu ukawapo na kwa wengine kama anavyosema kwa wabunge,”alisema Simbachwene. 


Simbachawene aliwataka Tacaids kurudia tena kwa sababu wana kazi ya kufanya badala ya kuishia kutoa sababu zingine zikiwamo za kijiografia. “Mje na sababu za kitafiti na mfanye comparison (ulinganishi) na mikoa mingine maana pale (Njombe) huwezi kukuta watu wamejazana jazana kama ilivyo katika maeneo mengine nchini,”alisema. 

Naye Mbunge wa Mtambile(CUF), Masoud Abdallah Salim, alitolea mfano kuwa kwa Mkoa wa Dodoma kuwa maambukizi yanaonekana yamepanda, hivyo ufanyike utafiti kujua eneo gani limesababisha hali hiyo. “Ufanyike utafiti kama ni hapa kwetu bunge au kama vyuoni ili tujue Dodoma ni kitu gani kimepandisha maambukizi haya,”alisema. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Ukimwi na Dawa za Kulevya, Oscar Mukasa, alisema kama bunge wanapanga kuzindua utashi wa kisiasa ili kuonyesha kuwa wako mstari wa mbele katika kuunga mkono suala hilo. 

“Tarehe 20 mwezi huu baada ya serikali kuzindua upimaji Virusi vya Ukimwi kwa wanaume, Juni 19 sisi kama bunge tunazindua suala hili na kulibeba kuwa utashi wa kisiasa. 

Tumeshirikiana na Tacaids na wadau wengine tuone namna gani tunawaonyesha Watanzania kuwa bunge liko mstari wa mbele na namna tutakavyolitekeleza jambo hili,” alisema mwenyekiti huyo. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, aliahidi kuzingatia yote yaliyoelezwa na wabunge na kufanyia kazi. 

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini wa Tacaids, Dk. Jerome Kamwela, alisema miongoni mwa sababu ya kiasi kikubwa cha maambukizi ya VVU ni mikoa hiyo kuwa katika lango la kuingilia nchi zilizoko kusini mwa Afrika. Contact us Advertise Capital Radio East Africa Radio ITV Lokopromo X 6/8/2018 Wataka 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko. Alisema: “Kinachopimwa ni watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa wakati huo, haijalishi walipimwa lini, si kipimo sahihi kuwa ukimwi unashuka ama unaongezeka. 

Agosti au Septemba tutakuwa ripoti kamili ambayo sasa itatoa takwimu wangapi wamekufa na maambukizi mapya yakoje kwa kuwa ndo mara ya kwanza tumefanya kwenye eneo hili.” Kuhusu makundi maalum kupimwa kwa lazima, Dk. Maboko alisema kisheria bado suala la upimaji ni la hiari na lazima upimaji ufanyikwe katika kituo cha afya.

No comments

Powered by Blogger.