Full-Width Version (true/false)


Waarabu Wamchukua Zinedine Zidane Kwa Bilioni 133.7 Kwa Mwaka

IKIWA ni siku moja tu baada ya kujiuzulu kuwanoa Mabingwa wa Ulaya mara tatu mfulurizo, Real Madrid ya Hispania, kocha Zinedine Zidane amehusishwa kuajiriwa kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Qatar ambao ni wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022 baada ya Waarabu hao kuweka ofa mezani ya kumlipa Pauni milioni 44 (zaidi ya Tsh bilioni 133.7) kwa mwaka.

 Zidane mwenye umri mwa miaka 45, amejizolea umaarufu na heshima kubwa baada ya kuipa kuchukua UEFA Champions League mara zote akiwa kocha huku akichukua Laliga mara moja na makombe mengine.

Mfaransa huyo anatarajiwa kulipwa mkwanja wa pauni 120,000 kwa siku ambapo kwa miaka minne atakuwa amejikusanyia Jumla ya pauni milioni 176 kutoka kwa matajiri hao wa mafuta duniani.

Mmoja wa mabilionea wa Misri, Naguib Sawiris ameandika kuhusu ujio wa Zidane Qatar.


Timu ya Taifa ya Qatar itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki fainali hizo tangu mwaka 1934 walipofuzu kwa mara ya mwisho. Zidane ndiye anatazamiwa kuwapaisha waarabu hao katika kufikia hatua nzuri kwenye fainali hizo za kihistoria.Zidane alikuwa akipewa nafasi kumrithi Kocha wa Chelsea, Antonio Conte huku Jurgen Klopp akihusishwa kuchukua mikoba za Zidane Real Madrid pale Bernabeu.

 Mauricio Pochettino naye anapewa nafasi kubwa ya kuziba pengo la Zidane lakini tayari ameshasaini mkataba mpya wiki jana, maana yake Real Madrid watatakiwa kulipa pauni milioni 42 kumng’oa Mu-Argentina huyo kutoka Tottenham.

No comments

Powered by Blogger.