Full-Width Version (true/false)


Wabunge wahoji kukatika katika ovyo kwa umeme nchini

  

Wabunge wamelalamikia kukatika katika kwa umeme katika maeneo mbalimbali nchini na kuitaka Serikali kutamka ni lini watatua tatizo hilo. 

Wabunge hao ni Tunza Malipo (Viti maalumu, Chadema), John Mnyika (Chadema), Oliva Semguruka (Viti maalumu CCM)' Mbaraka Dau (Mafia CCM) na Lucy Owenya (Viti Maalum,Chadema) Akiuliza swali bungeni leo Juni 6, Tunza amehoji tatizo la kukatika katika kwa umeme mara kwa mara litaisha lini katika Mkoa wa Mtwara. 

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema Serikali kupitia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) limekamilisha ukarabati wa mitambo minane. Amesema mzabuni wa Kampuni ya Mantrac anaendelea na kazi ya ukarabati wa mtambo mmoja uliosalia na huenda ukakamilika Juni. 

Akiuliza swali Mnyika amehoji kuna tatizo la kukatika katika kwa umeme na kupunguza kwa kiasi cha umeme katika jimbo lake la Kibamba na kuhoji ni lini watarekebisha hilo. 

 Akijibu swali hilo, Subira amesema kuna hatua mbalimbali za kutatua tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha kupozea umeme katika jimbo la Kibamba.

No comments

Powered by Blogger.