Full-Width Version (true/false)


''Wachezaji hawana mpango na timu ya taifa''Winga wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa huko Afrika Kusini, Uhuru Seleman, amesema timu ya taifa ya huko haifanyi vizuri kwa sababu wachezaji hawana mpango na timu hiyo. 

Uhuru ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na eatv.tv, ambapo ameeleza kuwa chanzo cha timu ya taifa ya Bafanabafana kutofanya vizuri licha ya kuwa na huduma zote nzuri ni kutokana na wachezaji kutothamini timu hiyo.

Wachezaji wa kule hawajali kabisa timu ya taifa, wanaona kama sio ya kwao, wanachojali ni kuchezea klabu zao na  kuwafurahisha mashabiki wa timu zao kuliko kuchezea timu ya taifa, wanaona kama haiwahusu'', amesema.

Uhuru ameongeza kuwa wachezaji wengi wa Afrika Kusini hupenda kucheza soka la kufurahisha mashabiki wa klabu zao tu na hawana uchungu hata wakikaa benchi kwani malipo yao yapo palepale na wanalipwa vizuri.

Aidha Uhuru amesema suala hilo haliishii kwa wachezaji pekee, bali hata viongozi wa vilabu hawapendi michuano ya nje ya Afrika Kusini kwani wanaamini ligi yao inawalipa vizuri kuliko michuano ya kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.