Full-Width Version (true/false)


Wachezaji wa Simba kupewa milioni 66 endapo watachua kombe la Sportpesa

 

Hatimaye klabu ya Simba imefunguka na kusema fedha zote za ubingwa wa Sports Pesa Super Cup watapewa wachezaji.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema fedha zote dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 66) kama watabeba ubingwa zitakuwa mali ya wachezaji.
 

“Tayari tumezungumza nao na kuwaeleza kuhisiana na suala hilo kwamba fedha zote zitaenda kwao,” alisema.
 

Manara amesema hayo mara tu baada ya Simba kushinda kwa mikwaju ya penalti na kutinga nusu fainali.
 

Simba imeing’oa Kariobang Sharks kwa penalti 3-2 baada ya mechi kwisha bila bao katika dakika 90.


No comments

Powered by Blogger.