Full-Width Version (true/false)


Wakongwe tumesharudi, hatuwezi kukubali – Juma Nature

Msanii wa Bongo Flava, Juma Nature amesema wasanii wa muziki huo waliochipukia miaka ya hivi karibuni baadhi yao wamekuwa wenye kubweteka mapema.
Juma Nature ameiambia FNL ya EATV kuwa kitu hicho sio sahihi kwani muziki ni kazi ingawa wengine wanachukulia kama ubishoo.
“Wasanii wanabweteka sana na hilo ndio tatizo kubwa la vijana wa sasa hivi akitoa wimbo mmoja anajiona ameshaweza kila kitu,” amesema. 

Nawaambia kitu kimoja kwamba wakongwe tumesharudi na hatuwezi kukubali kuona wanakuja watu wengine kutoka sehemu zingine watupite tunawaona hivi hivi, sikubali hata kidogo”, amesisitiza.

Juma Nature ameongeza kuwa wasanii wapo wengi ila wamekuwa na mtindo wa kuigana kitu ambacho kinaondoa ushindani, hivyo kuwataka wasanii kuacha uvivu katika kazi zao na kufanya ili kuwasaidia wao pamoja na vizazi vijavyo.

No comments

Powered by Blogger.