Full-Width Version (true/false)


Walimu wakuu wanaowalinda wanaowapa mimba wanafunzi waonywa.

 


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo, kuacha tabia ya kuwalinda baadhi ya wanaume wanaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi na kuwakatisha masomo yao kwamba wakigundulika watachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kuziagiza mamlaka zao za nidhamu kuwashusha madaraka mara moja. 

Mongella ametoa agizo hilo katika chuo cha ualimu Butimba wilayani Nyamagana wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wakuu 900 kutoka halmashauri nane za mkoa huo, maasa elimu wa wilaya, wathibiti ubora wa elimu mkoani humo pamoja na makatibu wa tume ya utumishi wa walimu. 

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka viongozi na watendaji wa sekta ya elimu mkoani Mwanza kuandaa mpango mkakati utakaotoa maelekezo kwa wazazi na walezi kuhusu utaratibu wa uchangiaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi shuleni kwa lengo la kuongeza ufaulu na kupunguza utoro miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi. 

Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza Michael Ligola amesisitiza umuhimu wa walimu wakuu kutunza nidhamu za wanafunzi katika shule zao.

No comments

Powered by Blogger.