Full-Width Version (true/false)


Wanaomiliki silaha wapewa wiki mbili kuziwasilisha polisi

Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limetoa wiki mbili kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuziwasilisha vituo vya Polisi ama Osi za Serikali za Mitaa kabla hatua kali za kisheria  kuchukuliwa dhidi yao. 
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara LUKAS MKONDYA na kusema silaha hizo zimekuwa zikitumika kuwinda wanyama kinyume cha sheria sambamba kufanya uhalifu wa aina mbalimbali. 
Aidha kamanda MKONDYA ametaka wenyeviti  wa serikali za mtaa, vijiji na watendaji wa vijiji na kata  kutoa ushirikiano katika oparasheni hiyo ili kuwabaini wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria katika maeneo yao.

No comments

Powered by Blogger.