Full-Width Version (true/false)


Wanyama afunguka tetesi za kwenda Liverpool
Kiungo wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama amesema tetesi zilizopo kuwa msimu ujao huenda akaonekana kwenye uzi wa klabu ya Liverpool si za kweli. 

Akiongea kwenye kipindi cha Shabiki On Saturday cha East Africa Television, Wanyama amesema hizo tetesi sio za kweli yeye bado ni mchezaji wa Tottenham na ataendelea kuwepo klabuni hapo.

''Mimi bado ni mchezaji wa Tottenham na nina mkataba na timu hiyo kwahiyo nipo pale bado hizo ni tetesi tu ila ukweli mimi nitacheza pale msimu ujao'', amesema.

Wanyama ambaye ni raia wa Kenya yupo nchini kwa mapumziko mafupi baada ya ligi kuu nchini England kufika tamati kwenye msimu wa 2017/18. Tottenham imemaliza katika nafasi ya 3 ikiwa na alama 77.

Kiungo huyo anayesifika kwa ukabaji, ameahi kucheza soka katika ligi tofauti tofauti ikiwemo Ubeligji anakocheza Mbwana Samatta pamoja na Scotland kabla ya kutua rasmi nchini England.

No comments

Powered by Blogger.