Full-Width Version (true/false)


Watano kuondoka kwa pamoja Singida United


Mkurugenzi wa Singida United FestoSanga amewataja wachezaji watano (5) wanaotarajia kuondoka baada ya kupata ofa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Mpira siku hizi umekuwa biashara jnaweza kuwa na mchezaji ameahidiwa dau la $5000 wakati wewe unamlipa $2000 anaweza kukubali kutumikia klabu yako lakini si kwa moyo kwa sababu ulimnyima nafasi ya kwenda kwenye maslahi bora zaidi.”

“Kuna wachezaji wengi ofa zao zimekuja kwetu na wataondoka. Danny Usengimana, Rusheshangonga Michele, Mudathir Yahya, Tafadzwa Kutinyu ameshajiunga na Azam hao ni baadhi ambao wamepata ofa za kununuliwa.”

“Shafiq Batambuze kuna watu wanamuhitaji, sisi upande wetu tunafurahi kwa sababu unapopata fursa ya kuuza mchezaji ni jambo zuri kwa sababu wachezaji wengi wa kiafrika mara nyingi wanakuwa hawana mwendelezo mzuri wa ubora wao.”

“Soko la sasa hivi la Kitinyu halitakuwa hivyo mwakani, anaweza kjwa vizuri leo mwaka ujao kiwango chake kikashuka na mkataba wake ukaisha matokeo yake anaondoka bure kwa hiyo inapotokea fursa ya kumuuza unauza haraka.”

Sanga amesema Kaseke pia ataondoka kwenda South Afrika ambako amepata timu iliyopanda daraja kucheza ligi kuu.

No comments

Powered by Blogger.