Full-Width Version (true/false)


Wazazi waanzisha mashamba kuzalisha chakula cha wanafunzi.
Baadhi ya wazazi wilayani Mufindi mkoani Iringa wameanzisha mashamba ya pamoja kwaajili ya kupata chakula cha wanafunzi shuleni ili kuwa na uhakika wa wanafunzi wao kupata chakula cha mchana shuleni. 

Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya Imehe iliyopo katika kata ya Nyololo wilayani Mufindi bwana Zuberi Nchimbi amesema kwenye mahojiano na mwandishi wetu  kuwa lengo la kuanzisha mashamba hayoni kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula kwa uhakika shuleni na pia kuondoa migogoro ya baadhi ya wazazi wasioweza kuchangia chakula moja kwa moja. 

Afisa elimu msingi wa wilaya ya Mundi Kennedy Bukagile amesema kwenye kilele cha wiki ya elimu wilayani humo iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Igowole kuwa uboreshaji wa mazingira pamoja na vifaa vya kujifunzia shuleni unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau ukiwemo mradi wa tusome pamoja umesaidia kupunguza idadi ya wahitimu wa darasa la saba wasiojua kusoma kuandika na kuhesabu. 

Akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri David William Asa Tawala wa wilaya hiyo Ndugu Joseph Mchina ametembelea maonesho ya elimu kujionea mbinu shirikishi zinazotumika na walimu yakiwemo madarasa yanayoongea chini ya mradi wa tusome pamoja unaofadhiliwa na Shirika la maendeleo la watu wa Marekani USAID.

No comments

Powered by Blogger.