Full-Width Version (true/false)


Waziri Mwigulu ameanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuwasikiliza Mahabusu na wafungwa.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dakta Mwigulu Nchemba amesema wizara yake imeanza utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa jijini Arusha kuhusu upatikanaji wa haki kwa Mahabusu waliopo gerezani kwa kubambikiwa kesi na wale wanaotumia muda mrefu gerezani bila kesi zao kusikilizwa kwa madai ya kutokukamilika kwa upelelezi.

Akizungumza jijini  Arusha katika gereza la mkoa wa Arusha la Kisongo katika ziara yake kutembelea magereza nchini Dakta Nchemba anasema tayari ameanza kuwasikiliza Mahabusu hao. 

Ama kuhusu maelekezo ya Rais Dakta John Pombe Magufuli ya kuyataka magereza yote kujitosheleza kwa chakula, Waziri Nchemba anasema maandalizi yote yameshakamilika yakiwemo ya upatikanaji wa zana za kilimo. 

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Hamisi Nkubasi ndiye mkuu wa jeshi hilo mkoa wa Arusha anasema wamejiandaa kuzalisha katika eneo walilonalo likiwemo gereza la Mang’ola lenye fursa ya umwagiliaji.

No comments

Powered by Blogger.