Full-Width Version (true/false)


Waziri Ummy awataka Watanzania kutowaficha watoto wenye maumbile tofautiWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka Watanzania watakapoona mtoto ana maumbile tofauti wawasiliane na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ili kuokoa maisha ya watoto huyo.


Ummy amesema kuwa watakapoona mtoto amezaliwa akiwa na maumbile ambayo hayajazoelewa wawapeleke katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kupatiwa msaada. 

“Naomba nitoe rai kwa Watanzania wote pale ambapo anazaliwa mtoto angalau labda ni tofauti na ilivyozoeleka wawalete hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili iweze kanavyo ili tuweze sasa kuhakikisha madaktari wetu bingwa wanatoa msaada ikiwemo kuwatenganisha. Kwahiyo tunaangalia kama tutawatenganisha ndani ya nchi au Nje ya nchi,” amasema Waziri Ummy, leo Juni 5, 2018 Bungeni jijini Dodoma.

Amesisitiza kuwa ” kwahiyo tusiwafiche watoto hawa, mtoto ambaye tunamuona anamaumbile tofauti wawasiliane na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ili tuhakikishe tunaokoa maisha ya watoto wetu.”

No comments

Powered by Blogger.