Full-Width Version (true/false)


Wema Sepetu Afanyiwa Oparesheni Arejea Nchini.... Meneja Wake Atoboa Siri ya Ugonjwa Unaomsumbua


Mwigizaji Wema Sepetu, amerejea kutoka nchini India ambapo alienda kwa matibabu.

Meneja wa mlimbwende huyo ambaye amewahi kutwaa taji la  Miss Tanzania 2006, Martin Kadinda amesema amerejea juzi, baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo.

“Wema amerejea lakini kwa sasa hawezi kuzungumza kwenye simu anahitaji kupumzika, amefanyiwa upasuaji mdogo na anaendelea vizuri,” amesema Kadinda.

Alipoulizwa kuhusu upasuaji huo, hakuwa tayari kuzungumzia kwa kina badala yake alijibu ni mambo ya wanawake.

“ Ninachoweza kukwamba ni kwamba ni upasuaji mdogo, ndiyo maana alikwenda pekee yake, tena natumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki wake kuwa Wema anaendelea vizuri kiafya,” amesema Kadinda.

Habari kuhusu matibabu ya Wema anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya, zilibainishwa wiki iliyopita baada ya kushindwa kufika mahakamani  Mei 29 ili kuendelea kusikiliza kesi yake.

Mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariamu Sepetu  alifika mahakamani hapo na kuijulisha kuwa mwanaye anaumwa yupo India kwa ajili ya matibabu.

 Mama huyo alilazimika kuwasilisha  nyaraka za kusafiria na kuzionyesha  kwenye Mahakama hiyo badala ya za matibabu.

No comments

Powered by Blogger.