Full-Width Version (true/false)


Wema Sepetu atamani ndoa ya Diamond na ZariMalkia wa Filamu Bongo, Wema Sepetu amempongeza Diamond Platnumz kwa ngoma yake mpya ya ‘Iyena’ aliyomshirikisha Rayvanny.


Katika maudhui ya ngoma hiyo, Diamond amecheza na Mzazi mwenzie Zarina Hassan (Zari The Boss lady) kama wamefunga ndoa, Wema amemtaka msanii huyo kufanya kweli.

“New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli. Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri,” ameandika Wema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kabla ya Diamond na Zari kuwa na mahusiano yaliyoplekea kuwa na watoto wawili na baadaye kutengana, Muimbaji huyo alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wema Sepetu.

siku ya wapendanao (Valentine Day) Zari The Boss Lady alitangaza kuvunja kwa mahusiano yake na Diamond kwa alichodai muimbaji huyo anavunja utu wake katika mitandao kwa kuwa na wanawake tofauti tofauti.

No comments

Powered by Blogger.