Full-Width Version (true/false)


Wolper amuumbua Hamonize kutumia jina lake kutapeli watu

 


Msanii wa filamu Jackline Wolper amekanusha kuwepo kwenye Shoo ya Harmonize ‘Kusi Night’ itakayofanyika Dar Live Sikukuu ya Eid pili, ambapo mrembo huyo ametajwa na Hamornize atakuwepo. 

Wolper amekanusha kupitia mtandao wa Instagram katika akaunti yake kwa kuandika hivi : “Naombeni mtambue kuwa sipo Tanzania na sitokuwepo kwenye shoo yoyote… iwe ya Mbagala iwe ya Posta, yote mnayoyasikia wanayasema ni ya uongo wanataka kuwatapeli, sitaki mtu atumie jina langu kuvuta watu. Epuka matapeli.” 

Baada ya muda Mwanamuziki Hamornize aliandika komenti hivi "Accaunt hii imehakiwa tena #ogopamatapeli" katika ukurasa huo wa Wolper ni kama amemjibu baada ya kukanusha. June 5, Hamornize alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa amemchangua Wolper kuongoza shoo hiyo.

“Wolper ana uwezo wa kuongoza shoo, kwa sababu ameshazoea sana mambo haya, pia ana mashabiki wengi. Ninaamini ataweza kuisimamia vizuri,” alisema. 

“Lengo ni kuwaonesha watu kuwa hatuna tatizo mimi na yeye na tunashirikiana katika kazi, hii yote tunaepusha kuwagawa mashabiki, yeye ana mashabiki zake na mimi nina wangu,” amesisitiza. 

Utakumbuka Harmonize na Wolper walikuwa katika bifu kitu kilichopelekea kutupiana maneno katika mitandao na kwenda mbali zaidi hadi kumhusisha mpenzi wa sasa wa Harmonize, Sarah.

No comments

Powered by Blogger.