Full-Width Version (true/false)


Yafahamu haya mabadiliko ya Kombe la Dunia
Zimebaki siku 6 kabla ya fainali za Kombe la Dunia 2018 kuanza huko nchini Urusi, ambapo kipenga cha kwanza kitapulizwa Alhamisi ya Juni 14 saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, pale wenyeji Urusi watakapokipiga na Saudi Arabia. 

Kabla ya fainali za mwaka huu tayari zimeshachezwa fainali 20, tangu zilipoanzishwa rasmi mwaka 1930, na kwa mara ya kwanza kushirikisha timu 13 pekee na bingwa wa kwanza kuwa Uruguay.

Baada ya hapo fainali hzio zimekuwa zikipitia mabadiliko mbalimbali ikiwemo kuongezwa kwa idadi ya timu zinazoshiriki na bara la Afrika kupata timu tano kutoka mwakilishi mmoja wa kwanza ambaye alikuwa ni Misri katika fainali za mwaka 1934.

Mwaka 1930 zilishiriki timu 13 huku mchezo wa fainali zikicheza timu za Uruguay na Argentina, ambapo wenyeji Uruguay walishinda kwa mabao 4-2. Mwaka 1950 ziliongezeka timu na kufikia 16, kabla ya Mwaka 1982 kufikia timu 24.

Mwaka 1998 kwa mara ya kwanza zikashiriki timu 32 na fainali hizo zilifanyika nchini Ufaransa na wenyeji kuibuka mabingwa kwa kuwafunga Brazil kwa jumla ya mabao 3-0. Tayari FIFA imeshafikia makubaliano ya kuongeza hadi timu 48 kwenye fainali za mwaka 2026.

No comments

Powered by Blogger.