Full-Width Version (true/false)


Yanga kumsajili kipa wa Mtibwa Sugar, Benedict Tinocco

Mlinda mlango wa Mtibwa Sugar, Benedict Tinocco ameaga ndani ya kikosi hicho na msimu ujao wa ligi kuu anadaiwa atakuwa kwenye timu moja mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. 

Tinocco ambaye amesajiliwa na Mtibwa akitokea Yanga na kupata msasa chini ya Kocha Patrick Mwangata anayetwaja kuwa bora katika kuwanoa walinda mlango. Inadaiwa yupo kwenye mazungumzo na timu tofauti ikiwemo Simba lakini Yanga ndiyo wako kwenye nafasi ya kumchukua mchezaji huyo na muda wowote atasaini. 

Jamaa wa karibu wa Yanga amesema, kikosi hicho kinamuhitaji mchezaji huyo kwa nguvu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu. "Zipo timu nyingi zinazomuhitaji lakini Yanga ni miongoni mwa timu hizo na inamuhitaji kwa nguvu zote, ingawa zipo pia KMC na nyingine,"alifafanua jamaa huyo. 

Hata hivyo, alipoulizwa Tinocco amesema: "Mimi nimeaga Mtibwa lakini si kwa sababu naenda Yanga, kuna mipango yangu mingine ninayotegemea kuifanya kama hizo habari zipo tusubiri tuone." 

Tinocco amesema, kuna timu tofauti zinazohitaji huduma yake hasa baada ya kusikia amemaliza mkataba wake na Mtibwa lakini hawezi kuweka wazi hadi mipango itakapokamilika.

No comments

Powered by Blogger.