Full-Width Version (true/false)


Yanga yaja na mikakati ya nje ya uwanja


 

Uongozi wa Yanga umesema haupo tayari kurudia makosa ya msimu uliopita na kubainisha kuwa msimu ujao hawatakuwa na sababu ya kwani wameshindwa kutwaa ubingwa nje ya uwanja. 

Yanga msimu huu wameshindwa kufanya vizuri kutokana na wachezaji wao wengi tegemezi kushindwa kuisaidia timu kutokana na majeraha yaliyowaweka nje muda mrefu. 

Meneja wa klabu hiyo, Hafidh Saleh alisema hawana presha ya kusajili kwa sasa wanasajili taratibu na kwa umakini zaidi ili kukwepa changamoto ya kujaza majeruhi katika kikosi chao kipya. Alisema pia usajili wao unalenga zaidi kuziba nafasi zilizokuwa na matatizo msimu uliopita huku akiweka wazi kuwa hawasajili kutokana na upepo wa wachezaji waliofanya vizuri msimu huu bali wanafuata ripori ya mwalimu inasemaje. 

"Unajua kumekuwa na maneno mengi kuwa Yanga msimu huu haina fedha na ndio maana haifanyi usajili siyo kweli tunaangalia kwa umakini na tupo katika mikakati imara zaidi kuhakikisha tunafanya usajili bora zaidi kulingana na mahitaji," alisema. 

Saleh alisema "msimu uliopita tulikuwa tunakabiliwa na majeruhi wengi ndio walikuwa wachezaji tegemezi katika kikosi jambo ambalo lilisababisha kushindwa kuionyesha ushindani hivyo kwasasa tunaangalia mambo mengi kabla ya kumsajili mchezaji kwa lengo la kukwepa changamoto hiyo,". 

Yanga hadi sasa wamesajili mshambuliaji, beki na kuwaongeza mikataba wachezaji wake waliokuwa wamemaliza mikataba akiwemo Kelvin Yondan.

No comments

Powered by Blogger.