Full-Width Version (true/false)


Yanga yalazimishwa sare na Mbao FC


Kikosi cha Yanga "B" kimelazimishwa sare ya 0-0 na Mbao FC katika mashindano ya Uhai CUP kwenye mchezo kundi A uliopigwa jijini Dodoma kwenye Uwanja wa UDOM Info leo.
Kikosi hicho kimebanwa na Mbao FC kwenye mchezo wa kundi hilo na kushindwa kuwashusha wapinzani wao walio juu ya kilele kwenye kundi hilo.
Mbali na matokeo hayo, mechi zingine zilizopigwa hii leo katika kundi C ni Ruvu Shooting FC wa dhidi ya Mbeya City, ambapo Ruvu imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja, bao pekee la mchezo huo limefungwa na Abdallah Mgemwa, dakika ya 21.
Aidha, Mtibwa Sugar nayo ilifanikiwa kuitandika Mwadui FC kwa jumla ya mabao 3-1, mabao yakifungwa na Omary Sultan, Richard Mwamba na Onesmo Justine huku bao pekee la Mwadui likifungwa na Frank Mushi.

Mechi nyingine ya kundi C iliwakutanisha Majimaji FC na Azam FC kwenye Uwanja wa Udom Social ambapo iliweza kwenda sare tasa ya 0-0.

No comments

Powered by Blogger.