Full-Width Version (true/false)


Yanga yaweka kando agenda ya Uchaguzi


 Kuelekea Mkutano mkuu wa Yanga Juni 10 mwaka huu, uongozi umeweka wazi ajenda kuu zitakazojadiliwa huku ajenda ya uchaguzi ikiwa imewekwa kando kwanza.Maandalizi ya mkutano huo kwa wanachama wa Klabu ya Yanga yameshika kasi sasa zikiwa zimesalia siku nne kuelekea mkutano huo muhimu utakaotoa dira kwa klabu hiyo.

Akielezea masuala mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wako hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa maofisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

"Tunatarajia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo Yusuph Manji ambaye alikua mwenyekiti na mfadhili wa klabu hii, Baraza la Michezo,TFF  pamoja na wizara husika,"amesema Mkwasa.

Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema mkutano huo utakuwa na lengo la kuwaeleza wanachama matatizo yanayoikabili timu yao, kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi zililizo wazi utatangazwa baadaye.

No comments

Powered by Blogger.