Zoezi la kuaga miili ya Maria na Consolata limeazna Iringa
Miili ya
pacha walioungana
Maria na Consolata
imewasili kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha Iringa
(Rucu).
Tukio la kuagwa kwa pacha hao limetangazwa kuwa ni la kitaifa na
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ameeleza kuwa Rais John
Magufuli ni miongoni mwa walioguswa na kuhuzunishwa na vifo hivyo.
"Huu ni msiba wa kitaifa Rais angehudhuria ila amebanwa na ratiba
Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri Ofisi ya
Rais, Sera, Bunge na Walemavu, Stella Ikupa wataudhuria hapa,"
amesema Kasesela.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, Abdul-Razaq Badru ni miongoni mwa
watu waliohudhuria akaeleza kusikitishwa na vifo hivyo kwa kuwa
vimezuia pacha hao kutotimiza ndoto zao za kuwa wanataaluma.
Anatumia nafasi Hiyo kuwasihi wanafunzi kutambua mikopo
inayotolewa ni rasilimali muhimu, Serikali inalenga kuwawezesha ili
wawe wataalam watakaosaidia nchi
No comments