Full-Width Version (true/false)


Achapwa viboko 80 kwa kunywa pombe

Leo July 12,2018 nakusogezea stori hii kutoka huko nchini Irani ambapo Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la ‘M R’ amechapwa viboko 80 hadharani kwa kosa la kunywa pombe wakati akiwa na umri wa miaka 14.

Waendesha mashtaka wamesema kuwa ‘M R’ alikamatwa wakati wa maadhimisho ya mwaka wa Iran wa 1385 wa kati ya (March 2006 na March 2007) na alihukumiwa mwaka uliopita.

Shirika linalodili na masuala ya haki za kibinadamu la Amnesty International limelaani vikali kitendo hicho kwa madai ya kukiuka misingi ya Kibinadamu.

Aidha bado haijajulikana sababu iliyochangia adhabu hiyo kuchukua zaidi ya miaka 10 kutekelezwa.

No comments

Powered by Blogger.