Full-Width Version (true/false)


“Afadhali ulime Bangi kuliko Kahawa”

Leo July 11, 2018 kutoka mkoani Kagera katika Jimbo la Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka amesikiliza kero za wananchi wake hasa wa zao la Kahawa ambapo wamedai manyanyaso wanayoyapata katika zao hilo ni bora walime Bangi.

Akijibu hoja za wananchi wake Tibaijuka amesema kilio juu ya zao la Kahawa hata Rais Magufuli anafahamu kwani yeye kila anaposimama Bungeni anaongelea zao la Kahawa.

“Kila nikisimama Bungeni ni kahawa, sababu najua Wananchi wangu maslahi yao ni Kahawa hatuwezi jenga Shule, Zahanati bila kahawa, sasa Rais Magufuli hiki kilio amekisikia sababu sisi tupo watetezi wenu,” Prof. Tibaijuka

No comments

Powered by Blogger.