Full-Width Version (true/false)


Alex Sanchez wa Manchester United azuiwa kwenda Marekani

Mwanasoka wa kimataifa wa Chile anayeichezea Club ya soka ya Manchester United Alex Sanchez amezuiwa kuongozana na Wachezaji wenzake wa Old Trafford kwenda Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Tatizo ni nini? ni kutokana na kukosa VISA ya Marekani kulikotokana na kosa alilokutwa nalo February huko Hispania wakati akiichezea FC BARCELONA, imeelezwa kwamba alikutwa na hatia ya kosa la ukwepaji wa kodi na kuhukumiwa kwenda jela miezi 16.


Imeelezwa zaidi kwamba kwa sheria za Marekani, mtu aliyekutwa na makosa ya Mahakamani ni ngumu kupewa visa ya kuingia nchini humo hivyo Sanchez atakosa ziara hiyo ya Manchester United ikiwa ni ya maandalizi ya msimu wa 2018/2019.

No comments

Powered by Blogger.