Full-Width Version (true/false)


Aliyegundua madini ya Tanzanite apelekwa India kwa matibabu
Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, Mzee Jumanne Mhero Ngoma, ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili,  leo amenza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India.


Kwa mujibu wa binti yake, Bi. Asha Ngoma, mgunduzi huyo ameamua kusaka matibabu zaidi  baada ya kufanyiwa matibabu ili kuona kama anaweza kupona kwa uharaka zaidi.


“Mzee amekuwa akipatiwa matibabu tokea wakati ule Rais Magufuli  alipomzawadia pesa shilingi milioni 100 mwezi wa Aprili mwaka huu  ya matibabu wakati  uzinduzi wa ukuta unaozunguka machimbo ya madini Mirerani mwezi April mwaka huu.“Tunamshukuru sana Rais Magufuli kwani pesa hiyo tulipewa mara moja nasi tukaanza matibabu hapo nyumbani  na kwa kweli amemsaidia sana sana  na hapa India tunatarajia matibabu yatamsaidia zaidi”, alisema Bi. Asha ambaye ameongozana  na mjukuu wa Mzee Ngoma, Khalifa.

No comments

Powered by Blogger.