Full-Width Version (true/false)


Aliyesoma Jangwani alia na matokeo mabaya
Kitendo cha shule ya Kongwe ya Sekondari ya Jangwani kuwa katika orodha ya shule kumi zilizoshika mkia katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita, kimewashtua watu wengi  akiwamo mke wa mbunge wa Mbinga Mjini, Jiang Alipo.

Mke wa mbunge wa Mbinga Mjini, Jiang Alipo
Saa chache baada ya matokeo hayo kutangazwa, Jiang Alipo, ambaye ni mke wa mbunge Sixtus Mapunda, leo Julai 13,  ameandika katika ukurasa wake wa facebook na kusema:
“Jangwani yetu imekumbwa na nini? What happened to our skirts (nini kimetokea kwa sketi zetu za rangi za machungwa), siamini.”
Jiang amesema alisoma Jangwani kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia mwaka 1995 hadi 1998.
“Kila wakati najisikia furaha kuwa sehemu ya watu waliosoma Jangwani katika maisha yangu.Lakini leo nimehuzunika, mmetufanya nini dada zetu? Jangwani iko kwenye kumi za mwisho? Msituangushe.”alisema
 “Natama kama nikiamka leo nikiwa na miaka 13, nikiambiwa nichague shule niichague Jangwani tena! Jangwani Girls, sketi zetu za machungwa zinaingia madoa, njooni tuungane tuokoe shule yetu, njooni tutafute suluhisho,” alisema
Alipo amesema wakati akisoma shule ya msingi Keko Magurumbasi siku zote alitamani kuvaa sketi za rangi ya machungwa zinazovaliwa na sekondari ya Jangwani.
Ameeleza kuwa akiwa darasa la saba kwenye zile fomu za kuchagua shule alijaza Jangwani kuwa ya kwanza, kisha mwalimu wake mkuu alimwita na kumshauri abadilishe mpangilio ili uwezekano wa kufaulu uwe mkubwa maana kwa kuwa  "Jangwani wanachaguliwa waliofaulu vizuri.
"Nikakataa, kata kata (ubishi sijaanza leo). Wazazi wakanisapoti na Jangwani ikabaki kuwa chaguo langu namba moja,” amesema Alipo.
Amesema matokeo yalivyotoka akajikuta amechaguliwa Jangwani na alikuwa na furaha na alishonewa sare za shule wiki tatu kabla ya shule hiyo haijafunguliwa.
Amefafanua kuwa kwa miaka minne aliyosoma Jangwani alikuwa ni mwanafunzi mwenye furaha kuwa sehemu ya shule hiyo na kuchaguliwa kwake kwenda kidato cha tano na sita kulichangiwa zaidi na yeye kusoma shule hiyo.

No comments

Powered by Blogger.