Arusha:Wanawake wazuia Wanaume kuzika mwenzao
Taarifa kutoka katika kata ya mto wa Mbu, Arusha leo July 17, 2018
ni hii ya wanawake kukataa wanaume wasishiriki kwenye mazishi ya mama
anayejulikana kwa jina la Ruth kutokana nakudaiwa kuuawa kisha kubakwa
na watu wasiojulikana huku wakiwatuhumu wanaume wa eneo hilo kuhusika na
matukio hayo.
Wakati jeshi la polisi Arusha likithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mbunge wa jimbo hilo la Monduli Julius Kalanga
amesema wanawake hao wamefikia uamuzi huo baada ya matukio hayo
kukithiri huku akilitaka jeshi la polisi kuchunguza na kuchukua hatua.
“Pamoja
na kuwa ni mtu wa nane kuuawa wanawake wameonyesha hisia zao kwa
kudhani kwamba wanaume ndio wanaowauwa kwani tangu matukio haya yatokee
haijawahi kutokea mtu aliyehukumiwa kutokana na matukio haya” -Mbunge Kalanga
No comments