Full-Width Version (true/false)


Asilimia 66 ya Wanaume wamekubali Dangote aoe Wake zao


Stori kuhusiana ishu ya Tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote kutangaza kuwa yupo single na akitokea Mwanamke yupo tayari kumuoa zinaendele kushika headlines ambapo asilimia 66 ya wanaume wameubali kuachia wake zao waolewe na Dangote iwapo tu wataingiziwa fedha katika akaunti zao.

Wanaume hao walipiga kura katika swali lililoulizwa katika akaunti ya Twitter iwapo wako tayari uwaachia wachumba zao ikiwa Dangote ataingiza Mamilioni ya fedha ili aoe wachumba zao.

Katika kura hiyo asilimia 34 ya wanaume walisema hapana hawatakubali kupokea fedha hizo kwani fedha sio kila kitu katika mapenzi.

Juzi iliripotiwa kuwa Wanawake zaidi 800 wakiwamo wa hapa nchini wametuma maombi ya kutaka kuolewa na tajiri huyo.

No comments

Powered by Blogger.