Full-Width Version (true/false)


Azam yaamua kumtumia chilunda Kagame leo kama tishio kwa Simba


Uongozi wa klabu ya Azam FC kupitia kwa Ofisa Habari wake, Jafaar Idd Maganga, umesema utamtumia mchezaji wake, mshambuliaji, Shaban Idd Chilunda katika mchezo wa fainali ya KAGAME dhidi ya Simba SC.

Maganga ameeleza Azam walifikia uamuzi huo ili kukipa kikosi chao nguvu ya kukabiliana na Simba kutokana na mchango wa Chilunda ambaye ameonekana kuwa kwenye kiwango kizuri hivi karibuni.

Ikumbukwe Azam wamemalizana na klabu ya CD Tenerife anayochezea Faridi Mussa nchini Hispania na alitakiwa kuelekea huko lakini Azam wameongea na viongozi wa timu hiyo ambayo anapaswa kwenda kwa mkopo wakiomba atumike katika mchezo wa leo.

Baada ya kuandika barua hiyo, Chilunda sasa rasmi atakuwa sehemu ya mchezo wa kesho dhidi ya Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam majira ya saa 12 jioni.

Azam walifuzu kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya miamba wa Kenya, Gor Mahia FC huku Simba wakiifunga JKU kutoka visiwani Zanzibar kwa bao 1-0.

No comments

Powered by Blogger.