Full-Width Version (true/false)


Baada ya kula kipigo vs Azam, uongozi Simba wafunguka tena juu ya kutumia kikosi tofauti Kagame Cup


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, amefunguka kwa kueleza mambo kadhaa ya kupoteza KAGAME dhidi ya Azam.

Simba walishindwa kutwaa taji hilo kwa mara ya 7 kwa kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Azam katika Uwanja wa Taifa jana.

Kufuatia kipigo hicho, Manara amesema lengo la kutumia kikosi mbadala na kile kilichocheza ligi kuu msimu uliopita lilikuwa na maana yake katika timu.

"Kabla ya Kagame Cup tuliitisha Press Conference na kuwaeleza watanzania kikosi Kitakachotumika na kwanini baadhi ya Wachezaji hawatotumika."

" Tuliwaeleza pia faida ya Kuwatumia wachezaji wengine haswa wale wapya na wale wengine ambao hawakupata muda wa kucheza msimu Uliopita . sote tunakumbuka zile Lawama za baadhi ya wachezaji Kutocheza Leo tumeona faida yake."

" Yupo mtu atataka kazimoto aachwe? Au Rashidi Juma asiwemo katika timu? Kuna faida kubwa kwa Uamuzi Uliofanywa na benchi la ufundi ama hakika Utalipa. "

" Najua baadhi yenu ni Vigumu kuelewa ila kupanga ni kuchagua na chaguo lao ndio Uamuzi sahihi ambao muda si mrefu mtapongeza" amesema.

No comments

Powered by Blogger.