Full-Width Version (true/false)


Baraza la Mawazili Croatia watinga jezi za timu yaoFainali ya kihistoria inasubiriwa kwa hamu duniani pale miamba ya soka Croatia itakaposhuka dimbani dhidi ya Ufaransa keshokutwa Jumapili.
Joto la fainali hiyo limetua kwenye Baraza la Mawazili nchini Croatia, ambapo wamejikuta wakivaaa jezi za timu hiyo walipokuwa kwenye vikao vyao.
Mawazili hao wa Croatia walivaa jezi hizo za timu ya taifa ikiwa ni hamasa kwa timu yao kuhakikisha inanyakua ubingwa kwenye fainali hiyo ya Jumapili.
Waziri Mkuu wa Croatia, Andrej Plenkovic aliwapongeza wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa hatua ya fainali ambayo wameingia.
Pia aliwapongeza viongozi wa soka nchini humo kwa kuiwezesha timu hiyo kufika hapo ambapo watakutana na Ufaransa.
Taifa hilo limeweka rekodi kuwa miongoni mwa mataifa madogo kutinga fainali ya Kombe la Dunia kama ile iliyowahi kuwekwa na Uruguay mwaka 1950.

No comments

Powered by Blogger.