Full-Width Version (true/false)


Bei ya zao la Muhogo yashuka kwa kasi Kigoma

 

Wakulima wa zao la Muhogo wilayani  Kigoma  wameiomba serikali kuingilia kati ili kulinusuru zao hilo baada ya kuporomoka kwa kasi bei ya Muhogo kutoka shilingi 1,000 kwa kilo mwaka jana hadi shilingi 200  mwaka huu  hali  ambayo imesababisha baadhi ya wananchi kutoendelea kulima zao hilo linalostawi kwa wingi mkoani Kigoma na kuuzwa ndani na katika nchi jirani ambazo zimepunguza uhitaji. 

Wamesema katika kijiji cha Kidahwe wilayani humo kuwa bei ya zao hilo imekuwa ikiporomoka hali inayofanya kuendelea kupata hasara ambapo wameiomba serikali kusaidia kupata masoko ya nje baada ya masoko ya nchi za Burundi na Rwanda kuonekana kushuka. 

Shirika la maendeleo la viwanda vidogo nchini (SIDO) mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la maendeleo la nchi ya Ubelgiji  ENABEL wameanza kufanya kampeni ya kuhamasisha wakulima wa zao la Muhogo mkoani Kigoma kutumia teknolojia mpya ya kuongeza thamani ili kupata masoko  ndani  na nje ya nchi.

No comments

Powered by Blogger.