Full-Width Version (true/false)


Beki Yanga atua Singida united


Imeripotiwa kuwa uongozi wa Singida United umemalizana na mchezaji wa zamani wa Yanga, Rajab Zahir kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo ya Singida.

Zahir ambaye alikuwa akizicheza klabu za Mbeya City, Ruvu Shooting na Stand United imeelezwa amekubaliana kila kitu na mabosi wa Singida na sasa kilichobaki ni kusaini mkataba pekee.

Taarifa kutoka Singida United zinasema Zahri aliingia kwenye rada za walima alizeti hao tangu usajili wa dirisha dogo msimu uliopita akipendekezwa na aliyekuwa Kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm ambaye ametimkia Azam kwa sasa.

Licha ya Pluijm kumpendekeza, harakati za kupata saini yake hazikuweza kuzaa matunda lakini walipiga moyo konde na sasa kila kitu kipo tayari ambapo muda wowote kuanzia sasa Zahir anaweza akamwaga wino.

Singida United imeamua kuzidi kukiboresha kikosi chake kwa kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi tayari kwa maandalizi kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19.

No comments

Powered by Blogger.