Full-Width Version (true/false)


Billnas Amtolea Uvivu Steve Nyerere "Achana na Mimi Komedi Zako Peleka Majukwaani"

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva ambaye anafanya vyema na ngoma yake mpya ya ‘Labda’ amemtolea uvivu msanii wa Bongo movie Steve Nyerere na kumtaka apeleke komedi zake majukwaani.

Bifu kati ya Billnas na Steve Nyerere lilianza juzi baada ya Steve kumtolea maneno Billnas na kumuita Mariooo na maneno mengine ambayo yalipelekea wasanii hao kujibizana Kwenye Instagram.

Lakini sasa Billnas amemtolea maneno Steve na kumtaka aache kumfuatilia na kama nia yake ilikuwa ni kuchekesha watu kumpitia yeye basi amekosea ni bora angefanya komedi zake kwingine kwani alivuka mipaka ya utani.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amemtolea povu hili Steve Nyerere:

Komedi zake asilete Kwenye vitu vyangu mimi ile ni kazi yangu yeye kama anataka kufanya komedi si yapo majukwaa ya komedi?.

Halafu isitoshe mimi sio mtu ambaye nina Vibe naye yaani sina ukaribu naye kihivyo mambo hayo angefanya mtu kama Idris ingawa hata yeye kuna mipaka hawezi kuvuka”.

Lakini pia Billnas ametoa onyo kwa watu ambao wamekuwa wakimtania tania kuhusu ishu yake na Nandy tangu itokee:

 Hata kama mtu anakutania isiwe too much maana siku hizi naona watu watu wanapenda kunivaa vaa yaani unashangaa mtu from nowhere anamuandika Billnas”.

No comments

Powered by Blogger.