Full-Width Version (true/false)


Bocco wala hana presha pale Msimbazi
STRAIKA wa Simba, John Bocco wala hana presha na ndio kwanza anawashangaa na baadhi ya wachambuzi wanaodai, ongezeko la wachezaji katika kikosi chao kitawapoteza wengi katika ramani ya soka na pengine kuua vipaji vyao.
Bocco alisema wanaozungumza hivyo wanashindwa kujua kila mchezaji ana aina ya uchezaji wake, hivyo kocha ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa nani acheze kwa mechi ipi na nani akae benchi kwa manufaa ya timu yake.
Akizungumza na Mwanaspoti, Bocco alisema binafsi bado ana nafasi ya kuendelea kucheza kikosi cha kwanza hata kama wakisajiliwa washambuliaji zaidi ya hao kwa vile anajiamini ana uwezo, japo maamuzi ya mwisho amemwachia kocha.
Alisema usajili unaofanywa unamfurahisha kwani anaamini utakuwa na tija kutokana na timu hiyo kushiriki mashindano mengi hivyo kila mchezaji atakuwa na namna ya kumshawishi mwalimu ili aweze kucheza kikosi cha kwanza.
Bocco aliyeifungia Simba mabao 14 Ligi Kuu akiwa nyuma ya kinara Emmanuel Okwi aliyekuwa na mabao 20, aliongeza amekuwa akifuatilia michuano hadi ilipomalizika kwa kuwaangalia waliosajiliwa katika kikosi chao ili kujifunza vitu vingi na ameona umuhimu wa wachezaji waliosajiliwa kwa uwezo walionao.
Anasema si kwamba safu ya ushambuliaji waliyoiunda msimu uliopita ni mbovu baada ya ujio wa Meddie Kagere, Adam Salamba, habana bali ni kuwaongezea changamoto ili wapambane zaidi.

No comments

Powered by Blogger.