Full-Width Version (true/false)


Bongo Movie mjipange aisee!
KAMA kuna wasanii wa filamu bado wanaamini wanaweza kutumia sekta hiyo kujificha kufanya ubabaishaji wao, wamekwisha kwani tayari wameshtukiwa na sasa kutakiwa waanze kujiengua wenyewe ili kubakiza watu wa kazi.
Mchongo huo umefichuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyesema hayo juzi mjini hapa wakati akizundua Bodi ya Filamu Mkoa wa Manyara na kusema serikali haitarajii kuendelea kuwa na wasanii wa filamu wasio na ujuzi, weledi na ubobezi.
Waziri Mwakyembe alisema anataka kuona sekta ya filamu nchini ikisonga mbele na kuwa ajira inayowaingiza kipato wasanii wa kweli watakaosalia kupiga kazi.
Alisema soko la filamu nchini lipo juu kwa vile Tanzania inaongoza kwa kuzalisha filamu nyingi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Pia alisema Tanzania inashika nafasi ya pili nyuma ya Nigeria kwa nchi za Afrika zinazozalisha filamu, lakini wasanii wanatakiwa kuacha kujirahisisha katika soko la filamu kwa kuuza kazi zao kwa gharama za chini kwani sanaa hiyo ni ajira.

No comments

Powered by Blogger.