Full-Width Version (true/false)


BREAKING NEWS: baada ya mtibwa kumbania hatimaye Dilunga asaini SimbaKiungo aliyekuwa akiichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hassan Dilunga, amejiunga na mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 Simba SC kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Dilunga amezima ndoto za kuelekea Yanga kama ambavyo ilikuwa imeripotiwa awali akihusishwa kuelekea kwenye klabu hiyo yake ya zamani.

Awali kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya viongozi wa Simba na Mtibwa juu ya usajili wa Dilunga ambapo Mtibwa walikuwa wanaonekana kumbania wakimuhitaji lakini pande zote mbili zimefikia makubaliano.

Simba sasa imeonesha nia ya kutaka kuimarisha zaidi safu yake ya kiungo kutokana na kuwa na wachezaji wengi kwenye safu hiyo akiwemo Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Said Ndemla na wengineo.

Usajili umefanikiwa ukielezwa ni pendekezo la Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, kuomba aongezewe kiungo mwingine ili kukifanya kikosi cha Simba kuwa kipana zaidi kuelekea Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.