Full-Width Version (true/false)


BREAKING NEWS: rasmi Fei Toto aliyesaini Singida atambulishwa Yanga...Hatimaye kiungo  Feisal Salum Abdalah “Fei Toto” ametambulishwa rasmi na uongozi wa klabu ya Yanga.

Fei Toto kutoka JKU amejiunga na Yanga akisaini mkataba wa miaka mitatu ikiwa ni saa chache baada ya kutangazwa amejiunga na Singida United.


Singida United kupitia Mkurugenzi wao, Festo Sanga, leo mchana walimtangaza Fei Toto kuwa amejiunga nao wakionyesha picha wakati anasaini na kukabidhiwa jezi za Singida United.

Lakini leo, Yanga imemtangaza rasmi kutua Jangwani huku ikielezwa mkataba wa Singida United ulikuwa na matatizo.

Baadaye wakasambaza video zikimuonyesha akieleza alivyojiunga na Singida United lakini hivi punde atatambulishwa Yanga.

Pamoja na Fei Toto alionekana akizungumzia kwenye video kueleza alivyotua Singida United na ataitumikia msimu ujao.

Pamoja na kumsaini Fei Toto, Yanga pia imsajili Jaffar Kibaya kutoka Majimaji kwa mkataba wa miaka miwili.


No comments

Powered by Blogger.