Full-Width Version (true/false)


Breaking News: Waziri Mbarawa amtumbua Mkurugenzi wa maji Kigoma

Mkurugenzi wa maji safi na taka Mkoa wa Kigoma(KUWASA)Saimon Lukuga 

WAZIRI wa Mji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amemuondoa kwenye nafasi yake ya Ukurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Kigoma (KUWASA) Saimon Lupuga baada ya  kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

Mbarawa amefikia hatua hiyo baada ya malalamiko ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kuwa mamlaka hiyo na Bonde la Mto Tanganyika pamoja na wahandisi wa maji hawatoshi kwenye nafasi zao kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Kutokana na hatua hiyo Waziri Mbarawa amesema atamuagiza  katibu Mkuu kuandika barua ya uhamisho wa Mkurugenzi huyo kurejeshwa Dar es Salaam kuanzia leo.

No comments

Powered by Blogger.