Full-Width Version (true/false)


Chanzo cha mapato ya AL Shabaab chatajwa


Taasisi moja ya utafiti nchini Somalia imesema kwamba kundi la wapiganaji wenye itikadi kali la Al Shabaab lina mfumo bora wa ulipaji kodi ambao unasababisha kupata mamilioni ya dola kwa mwaka.


Kundi hilo la Alshabaab limekuwa likifanya mashambulizi ya kigaidi na maelfu ya watu kupoteza maisha, na kusababisha uchumi wa Somalia kuzorota, hali ambayo pia imeifanya nchi hiyo kuzalisha wakimbizi maeneo mbalimbali duniani.


Taasisi hiyo ya Hiraal imesema ingawa kundi hilo lenye itikadi kali linafanya shughuli zake tu katika maeneo ya kusini mwa Somalia, hulazimisha watu katika maeneo mengi ya nchi kulipa kodi, ikiwemo katika mji mkuu Mogadishu, ambao unashikiliwa na majeshi ya serikali.


Mkuu wa taasisi ya Hiraal Hussein Sheikh- Ali amesema kwamba wapiganaji hao wenye itikadi kali wamejipatia zaida ya dola za Kimarekani milioni 10 katika kipindi cha mwaka 2016 kutokana na kodi iliyotokana na mifugo.


''Al Shabaab kama kundi lingine la wapiganaji na la kigaidi limekuwa likikusanya fedha kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato. Lilianza kwa kukusanya mapato kidogo kutoka kwa watu waliokuwa wakiwaunga mkono ndani na nje ya nchi.


''Lakini kundi hilo lilipopanuka na kuwa kubwa walianza kujenga mfumo wao wa ukusanyaji ushuru katika maeneo yote ya Somalia'' anasema Hussein Sheikh-Ali.

No comments

Powered by Blogger.