Full-Width Version (true/false)


Chelsea: PSG kaa mbali na Kante

London, England. Chelsea imechimba mkwara mzito kwa kuwaambia Paris Saint-Germain kwamba wasijisumbue kabisa kuhusu N'Golo Kante kwa sababu wanachokifikiria ni ndoto za mchana.

The Blues wanafahamu wazi staa wake amekuwa gumzo na kuwindwa na wababe hao wa Ufaransa, hivyo wameamua kuweka mambo bayana kwamba hakuna pesa inayotosha kumng'oa Kante kutoka Stamford Bridge.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa kwenye mipango ya rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, huku mkurugenzi wa michezo Antero Henrique amekwenda mara kadhaa London katika kipindi hiki cha uhamisho wa majira ya kiangazi ili kuanzisha mazungumzo ya kumnasa Kante.

Lakini, kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri anataka kiungo huyo abaki kwenye kikosi chake na bilionea mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich yupo tayari kufanya anachotaka kocha wake. Al-Khelaifi anataka kutoa Euro 100 milioni kumnasa Kante kwenye dirisha hili.

No comments

Powered by Blogger.