Full-Width Version (true/false)


Chilunda atuma salamu Hispania
Mshambuliaji Shabaan Idd Chilunda ametuma salamu Hispania kwa kuibuka mfungaji bora wa mashindano ya Kombe la Kagame kwa kuichapa Simba 2-1 katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Chilunda aliyejiunga na CD Tenerife wiki hii alifunga bao lake la nane katika mashindano ya Kombe la Kagame katika dakika 32, akiunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Bruce Kangwa.
Chilunda hii amekuwa katika kiwango cha juu tangu msimu uliopita na uwezo wake mkubwa wa kuzifumania nyavu umeifanya klabu ya Tenerife.
Mkurungezi wa Ufundi wa CD Tenerife, Alfonso Serrano amesema kwa sasa wanasubiri kupata viza ya Chilunda ili ajiunge nao.
"Tuna matumaini makubwa na Chilunda, tumekuwa tunamfutilia kwa karibu anakipaji cha hali ya juu, anakuja hapa kucheza kikosi cha kwanza, na kama hatopata muda wa kucheza, atakuwa na kazi maalumu," alisema Serrano.
Chilunda sasa atajiunga na Farid Mussa katika timu hiyo ya Hispania na kuongeza idadi wachezaji wa Kitanzania wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.

No comments

Powered by Blogger.