Full-Width Version (true/false)


Croatia kwa raha zao

 

Moscow, Russia. Kocha wa timu ya Taifa ya Croatia, Zlatko Dalic amewaambia vijana wake wajivunie mafanikio ya kufika fainali ya Kombe la Dunia 2018.

Dalic amewaambia vijana wake kitendo cha kufika fainali ni cha juu sana na wanapaswa kujipongeza na kusahau kichapo cha mabao 4-2 walichokipata kutoka kwa Ufaransa katika fainali iliyopigwa jana Uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow.

Alisema anaamini kuwa walipoteza mchezo huo kutokana na mwamuzi kutokua makini kwa kuwazawadia Ufaransa penalti iliyobadili mchezo wao.

“Mwamuzi alitutoa mchezoni mapema asingeipa Ufaransa penalti nadhani tungeweza kuwa mabingwa,” alisema kocha huyo.

Alisema wachezaji wanapaswa kujipongeza na kuangalia nini wataifanyia Croatia katika michuano ijayo ikiwemo ya Euro, badala ya kujadili kipigo.

“Hatua tuliyofikia ni ya juu sana, wakati tunafika hapa hakuna aliyekua akitupa nafasi ya kufika japo robo fainali, kwa hiyo hatua tuliyofika ni ya juu na mafanikio makubwa.”
Alisema sio nia yake kulalamikia uamuzi wa mwamuzi, lakini hadhani kama ni sahihi kutoa penalti ya kulazimisha katika mechi kama hiyo ya fainali.

No comments

Powered by Blogger.