Full-Width Version (true/false)


Dereva wa lori akamatwa na kilo 80 za bangi Shinyanga
Jeshi la polisi, Shinyanga linamshikilia dereva wa lori Emmanuel Chilunda (36) mkazi  wa Dar es salaam kwa kukutwa na magunia mawili ya bangi yenye uzito wa kilo 80, yakiwa yamechanganywa na marobota ya pamba.
Akizungumzia hilo leo Julai 10, Kamanda wa polisi Mkoani Shinyanga, Simon Haule amesema mtuhumiwa huyo, amekamatwa jana saa 7, mchana eneo la daraja la Manonga kijiji cha Isaka, wilaya ya kipolisi ya Msalala, Shinyanga.
Amesema mtuhumiwa huyo alitumia mbinu ya kuchanganya bangi na mizigo mingine ya pamba aliyokuwa amebeba kwenye gari hilo ili asibainike.
“Polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kufanikiwa kukamata gari hilo na baada ya kulipekua walikuta magunia hayo ya dawa za kulevya aina ya bangi,”amesema Haule
Kamanda Haule amesema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Hata hivyo, Haule ametumia muda huo kukemea vitendo vya baadhi ya wananchi kujihusisha na biashara haramu ya bangi ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu na yanadhoofisha jitihada za serikali za kukuza uchumi.No comments

Powered by Blogger.